Nimemsikia Mohammed Aboud Mohammed, anasema wananchi wasiwe na hofu na idadi kubwa ya wanajeshi, akidai kuwa wapo katika mafunzo yao ya kawaida na hawahusiani na Uchaguzi isipokuwa tu mafunzo yao yameingiliana na kipindi cha uchaguzi.
Naweza kukubaliana na kauli ya Aboud (kama si ya kisiasa), lakini kama
Serikali inayojali uhuru na haki za raia wake wanalazimika kutoa TAMKO
lenye uzito unaostahiki, kuwahakikishia wananchi wake amani na utulivu
na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida bila kuwawekea mipaka
ya muda wakati hawajavunja sheria za nchi.
"Serikali inayowaogopa wananchi wake ni Serikali ya KIDIKTETA"!
"Serikali inayowaogopa wananchi wake ni Serikali ya KIDIKTETA"!
No comments:
Post a Comment