Wajumbe wa Baraza la wawakilishi jana wamemchagua Zuberi Ali Maulid kuwa Spika wa baraza la wawakilishi.
Zuberi ametetea tena nafasi yake ya uspika kwa kipindi chake cha pili kuliongoza baraza hilo.
Zuberi alipata kura 70 ambazo alipigiwa kura na wajumbe wote wa baraza hilo ambao walikua 70.
Spika huyo aliwabwaga wagombea wenzake wanne ambao wawili pia waligombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi uliopita wa Octoba 28 mwaka huu.
Wagombeahao ni Hamad Mohd kutoka chama cha UPDP, katika uchaguzi wa uspika hakupata kura na Ameri Hassan Ameri kutoka chama cha Demokrasia makini ambae pia alikua mgombea Urais wa Zanzibar nae pia hakupata kura.
Wagombea wengine waliogombea nafasi ya Uspika ni Ali Makame kutoka chama cha CUF na Naima Salum Hamadi kutoka chama cha UDP ambao na wao hawakupata kura hata moja.
No comments:
Post a Comment