Vikosi vya Marekani vimeshindwa kuzuia kombora lolote la jeshi la IRGC la Iran lililorushwa dhidi ya kambi za Marekani nchini Iraq. Naibu mkuu wa operesheni wa jeshi hilo Brigedi Jenerali Abbas Nilforoushan amesema makombora ya Iran yamelenga kambi hizo kwa usahihi. Pia amesema majeshi ya Marekani japokuwa yamejiandaa vizuri kabla ya mashambulizi ya Iran, lakini wameshindwa kabisa kuzuia kombora lolote.
No comments:
Post a Comment