AFRIKA MASHARIKI YAONDOKEWA NA MWANAZUONI SHEIKH HARITH SWAALEH AL MAAWY (1937 - 2020)
Kenya inaomboleza kifo cha msomi maarufu wa dini ya Kiislamu Sheikh Harith Swaleh aliyefariki siku ya Jumatano na kuzikwa siku ya Alhamisi mjini Mombasa Kenya.
Sheikh Harith Swaleh aliyezaliwa mwaka 1937, mjini Lamu ametoa mchango mkubwa kwa jamii ya Waislamu Afrika Mashariki na Afrika ya Kati
Ni mwana wa chuoni ambaye amesomesha wasomi wengi maarufu wa dini ya Kiislamu ambao wengi wao wamekuwa wanazuoni maarufu.
Kati yao ni Sheikh Ahmed Msallam,, Sheikh Sayyid Athman Saggaf,, Sheikh Muhammad Sharriff Famau miongoni mwa wengi wengineo.
Marehemu Aliandika vitabu vya dini maarufu Utangulizi wa Tafsiri ya QURAN, Hadithi za Mtume Muhammad S.A.W na vitabu vinginevyo.
No comments:
Post a Comment