WELCOME
Translate
Sunday, November 8, 2020
HATIMAE BARAZA LA WAWAKILISHI LAPATA SPIKA MPYA FUWATILIA BLOG YETU KWA HABARI ZAIDI
Saturday, May 16, 2020
JIPATIE PESA UKIWA NYUMBANI
Sunday, March 15, 2020
M/MUNGU AMFANYIE WEPESI SHEE WETU HUSSEN NYUNDO
Friday, February 14, 2020
KITUKO DUNIANI JAMAN
Afisa mmoja wa utalii nchini Afriika Kusini ambaye alifanikiwa kupata picha isio ya kawaida ya nyani akimbeba mwana wa simba katika mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Kruger, amesema kwamba hajawaona tena wanyama hao tangu alipowapiga picha hiyo wiki iliopita.
Katika taarifa kwa BBC, mkurugenzi wa Kurt Safari , alisema kwamba msimu wa mvua umefanya kuwa vigumu kuwaona wanyama hao.
''Ni msimu wa mvua katika mbuga ya Kruger na miti imekuwa mikubwa huku nyasi zikiwa ndefu. Wakati nyani wanapoondoka katika barabara na kuingia katika nyasi , sio rahisi kuwaona''.
Sunday, February 9, 2020
BALAA YA MZIGE YAKARIBIA TZ
Thursday, January 9, 2020
INALILAH AFRICA MASHARIKI YAONDOKEWA NA MWANAZUONI WAKE
KESHO KUTAKUWA NA HALI YA KUPATWA MWEZI
MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO
Rais wa Marekani Donald Trump ameihakikishia nchi yake kuwa wakati wa utawala wake ataidhibiti Iran isiendelee na mpango wake wa nyuklia, akiitaja kuwa nchi inayofadhili ugaidi.
Akilihutubia taifa hilo jana, ikiwa ni siku moja tangu Iran ishambulie kambi mbili za jeshi la Marekani zilizoko nchini Iraq kama hatua ya kulipa kisasi cha kuuawa kwa kamanda wao, Qassem Soleimani, Trump amemuelezea kamanda huyo kama ‘gaidi hatari zaidi duniani’.
“Kama Mkuu wa Jeshi la Quds, Soleimani alihusika katika mashambulizi mengi, mikono yake ilikuwa imejaa damu za Wamarekani na Wairan na alitakiwa kuwa ameuawa siku nyingi zilizopita,” alisema Rais Trump.
“Kumuua Soleimani kumetuma ujumbe kwa magaidi wote duniani kuwa kama unathamini maisha yako mwenyewe hautatishia maisha ya watu wetu,” aliongeza.
Trump alisema kuwa Kamanda Soleimani alikuwa amepanga kufanya mashambulizi megine dhidi ya Wamarekani.
Katika hatua nyingine, Trump alisema kuwa mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na majeshi la Iran kwenye kambi za kijeshi za Marekani hayakuwa na madhara yoyote.
Alidai hakuna mtu aliyefariki na hakukuwa na aliyepata majeraha makubwa. Kwa mujibu wa wake, Jeshi la Marekani lilipata taarifa mapema kuhusu kufanyika kwa mashambulizi hayo na likachukua tahadhari zote.
Lakini taarifa hiyo ya Rais Trump inakinzana na taarifa iliyotolewa na Iran, ambao wameeleza kuwa mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya ‘magaidi 80 wa Marekani’.
Iran imeapa kuendelea kulipa kisasi dhidi ya hatua za Marekani. Kifo cha Kamanda Soleimani ambaye anaheshima kubwa nchini Iran kama mwanamapinduzi na shujaa kimeamsha hasira za nchi hiyo, akizikwa na maelfu.
Iran, imetangaza rasmi kuvunja mkataba wa mpango wa nyuklia kati yake ya Marekani, na inaendelea na uzalishaji kama kawaida.
Rais Trump alidai kuwa ili kuidhibiti Iran isiendelee na mpango wake wa Nyuklia, wataweka vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo; na kwamba Marekani inaweza kuishi bila kutegemea mafuta kutoka Mashariki ya Kati.
SHIDA KWA MMAREKANI
Wednesday, January 8, 2020
TRAMP ASEMA
MAREKANI YASHINDWA KUZUIYA KOMBORA DHIDI YA IRAN
MASHIRIKA YA NDEGE YASITISHA KUPITA KATIKA ANGA YA IRAN NA IRAQ
KIMENUKA SASA
Rais wa Iran, Hassan Rohani anatarajia kulihutubia taifa Jumatano wiki hii, hotuba ambayo itarushwa hewani moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Hotuba hiyo inakuja saa chache baada ya jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kurusha makombora kadhaa dhidi ya kambi mbili za jeshi zinazotumiwa na Marekani nchini Iraq.
Pentagon inasema kuwa karibu kambi mbili zilishambuliwa, mjini Irbil na Al Asad.
Tayari baadhi ya wananchi wa Iraq wamebaini kwamba mashambulizi hayo ya iran nchini Iraq yanavunja uhuru wa nchi yao.
Runinga ya kitaifa ya Iran imetangaza kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu Qasem Soleimani aliyeuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani mjini Baghdad, kufuatia agizo la rais wa Marekani Donald Trump.
Kuuwawa kwa Soleimani Januari 3 kulizorotesha uhusiano kati ya Iran na Marekani.
Jenerali Soleimani - alikuwa kiongozi wa oparesheni ya kijeshi ya Iran katika eneo la mashariki ya kati - lakini serikali ya Marekani ilimuona kuwa gaidi, ambaye alihusika na vifo vya mamia ya wanajeshi wake na kwamba alikuwa akipanga shambulio "hatari".
Tuesday, October 1, 2019
Tuesday, March 15, 2016
UDICTETA HAUFAI KWA RAIYA WENU KUWENI VIONGOZI WAADILIFU
Nimemsikia Mohammed Aboud Mohammed, anasema wananchi wasiwe na hofu na idadi kubwa ya wanajeshi, akidai kuwa wapo katika mafunzo yao ya kawaida na hawahusiani na Uchaguzi isipokuwa tu mafunzo yao yameingiliana na kipindi cha uchaguzi.
"Serikali inayowaogopa wananchi wake ni Serikali ya KIDIKTETA"!
Wednesday, October 28, 2015
KIMENUKA TENA ZANZIBAR
Friday, July 24, 2015
A HUNDRED YEARS FROM NOW
Yaa Allah give us strength to do righteous deeds,amen.
Wednesday, July 22, 2015
CHUO KIMOJA KIKUU NCHINI UWENGEREZA KIMESEMA KUWA UTAFITI WALIO UFANYA NYARAKA ZA ZAMANI KATIKA MAKTABA YAKE IMEONWSHA KUWA HUWENDA ZIKAWA ZA ZAMANI SANA
Chuo kimoja kikuu nchini Uingereza kimesema kuwa utafiti waliofanyia nyaraka za zamani katika maktaba yake, umeonesha kuwa huenda zikawa nakala za zamani sana duniani za koran. Watafiti katika chuo cha Birmingham wanasma kuwa walishangazwa sana walipogundua kupitia uchunguzi wa miale ya radiocarbon kuwa nyaraka hizo kutoka kitabu kitakatifu cha waislamu Koran, zina umri wa zaidi ya miaka 1300,
wanasema kuwa mwandishi wa nyaraka hizo huenda alikutana ana kwa ana na mtume Muhammadau alikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.
Nyaraka hizo ni miongoni mwa maelfu zingine za kale kutoka mashariki ya kati ambazo zilimilikiwa na mwana historia mzawa wa Iraq, Alphonse Mingana, aliyekabidhi kwa chuo kikuu hicho cha Birmingham katika miaka ya ishirini.
AWALI IDARA YA POLICE NCHINI KENYA ILIKUWA WAMETANGAZA KUWA ANGA YOTE YA KENYA ITAFUNGWA
Awali idara ya polisi nchini Kenya ilikuwa imetangaza kuwa anga yote ya Kenya itafungwa kwa muda wa siku tatu kabla ya ziara hiyo lakini kwa mujibu wa shirika la KCAA ndege zote zinazopaa chini ya futi elfu ishirini hazitaruhusiwa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyatta na uwanja wa wilson mjini Nairobi kuanzia siku ya Ijumaa hadi siku ya jumatatu, wakati wa kongamano la kimataifa ya ujasiriamali litakalofanyika mjini Nairobi.
Agizo hilo sasa linamaanisha ndege zote ndogo ndogo ambazo uhudumu kati ya Nairobi na Somalia na viwanja vingine vidogo vidogo katika kanda ya Afrika Mashariki, havitaruhusiwa kutua Nairobi hadi mkutano huo utakapomalizika.
Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa mjini Nairobi siku ya Ijumaa usiku ambapo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kibiashara kwa pamoja na mwenyeji wake rais uhuru Kenyatta.
SHIRIKA LA NDEGE LA KENYA LIMESEMA LITASITISHA SAFARI YAKE ZOTE ILI KUPISHA ZIARA YA RAISI OBAMA
Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa imetua.
Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.
LEO NDIO LEO MGOMBEA WA URAIS KUPITIA UKAWA LEO NDIO ANATANGWAZWA
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema mkutano mkubwa utakaofanyika Mwanza leo ndiyo utakaotegua nani atakayepeperusha bendera ya UKAWA katika nafasi ya Urais
Monday, July 20, 2015
RAIS J.KIKWETE AKIWEKA SAIN YA JARIDA LA MPANGO

WAZIRI WA SAYANCE AKISALIMIANA NA WACHEZAJI WA WAWI BOYS
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknlojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pro: Makame Mnyaa Mbarawa, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Wawi star, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya kuwania kombe la CCM jimbo la Wawi, dhidi ya Fidel castro, uliochezwa uwanja wa Gombani Chake chake Pemba, ambapo Fidel ilitazwa ubingwa (Picha na Haji Nassor, Pe
KUKOSEKANA MCHEZAJI SALUM ABDALLA KWENYE KOMBE LA CCM KATIKA JIMBO LA WAWI
KUKOSEKANA kwa machela maalumu kwenye michuano mbali mbali inayochezwa uwanja wa Gombani, husababisha kwa wachezaji kubebana wenyewe, kama juzi kwenye michuano ya kuwania kombe la CCM jimbo la Wawi, ambapo timu ya Wawi star ikimtoa mchezaji wao Salum Abdalla baada ya kupata majeraha, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MH MAKAME MNYAA AKISALIMIANA NA WAZAFUNZI WA FIDEL CASTRO PEMBA
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknlojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pro: Makame Mnyaa Mbarawa, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Fidel Castro, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya kuwania kombe la CCM jimbo la Wawi, dhidi ya Wawi star, uliochezwa uwanja wa Gombani Chake chake Pemba, ambapo Fidel iliibuka na ubingwa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKURUGENZI WA ZAWA ZANZIBAR NA MH BALOZI SEIF ALL IDD

KIONGOZI MAHIRI
